1 Chronicles 7:6-12

Wana Wa Benyamini

6 aWana watatu wa Benyamini walikuwa:
Bela, Bekeri na Yediaeli.
7Wana wa Bela walikuwa:
Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.
8Wana wa Bekeri walikuwa:
Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri.
9 bOrodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.
10Mwana wa Yediaeli alikuwa:
Bilhani.
Wana wa Bilhani walikuwa:
Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari.
11Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.
12 cWashupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.
Copyright information for SwhNEN